Burudani

Wasanii wa komedi kuungana na familia ya Sharo Milionea kufanya dua

Wasanii wa filamu za vichekesho nchini leo wataungana na familia ya marehemu Sharo Milionea kufanya dua. Leo ni mwaka wa pili tangu msanii huyo afariki kwa ajali ya gari.

sharo-milionea

Akizungumza na Bongo5 leo, Kitale aliyekuwa rafiki wa karibu wa msanii huyo alisema wasanii wa komedi wameona kuna kila sababu ya kwenda nyumbani kwa marehemu na kufanya dua hiyo.

“Unajua sisi ni wasanii ambao tulikuwa karibu na Sharo, sasa tukaona kwanini tusisafiri na kwenda Tanga kujumuika na wana ndugu wa Sharo na kufanya dua maalum kwaajili ya kumkumbuka mwenzetu! Hakuna kitu kikubwa zaidi ambacho tunaweza kukifanya kwaajili ya marehemu zaidi ya dua. Kwahiyo leo ndo safari ya kwenda Tanga na kufanya dua hiyo ambayo itahudhuriwa na wasanii mbalimbali wa komedi,” alisema Kitale.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents