Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

Wasanii wa Bongo Movie wanaishi ‘Ki Bongo Flava’ – Nikki wa Pili

By  | 

Msanii wa hip hop kutoka Weusi, Nikki wa Pili, ametia neno katika sakata linaloendelea la kupigwa marufuku kwa filamu za nje kwa madai zinaingizwa bila kulipiwa kodi hali ambayo imesababisha kuwa nyingi na kuzinyima filamu za ndani nafasi ya kufanya vizuri sokoni.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku ya Jumatano wiki hii baadhi ya wasanii wa filamu nchini kuandamana wakiwa na Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Paul Makonda, kupinga filamu hizo ambapo RC huyo alipiga marufuku filamu hizo huku akitaka wafanyabishara kufuata taratibu za kuziingiza nchini.

Baadhi ya wasanii wa filamu na muziki wamekuwa wakipingana na hatua hiyo ambapo Alhamisi hii, rapa Nikki wa Pili ameamua kutia neno kwenye sakata hilo.

“Nchi zote zilizoendelea zililinda masoko ya nyumbani, ndio tulilinde lakini wenye movie nao wajilinde kwa kujiongeza kila kukicha,” alitweet Niki wa Pili.

“Bongo Movies mwanzoni walikuwa na soko, kuanza ni kujaribu, but ku sustain is a science, mwendelezo wa lolote huitaji maarifa na maisha ya mwigizaji tofauti na mwanamuziki, Denzel na Jiga tofauti, sasa waigizaji wanaishi ki bongo fleva,” aliongeza.

Wasani wengine ambao walipinga maandamano hayo ni pamoja na Steve Nyerere ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit pamoja na Bella Fasta.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW