Bongo Movie

Wasanii wa filamu 10 waliofanya vizuri mwaka 2014

Bongo5 ikishirikina na wasambazaji na wauzaji wa filamu, inakuletea orodha ya waigizaji 10 waliofanya vizuri mwaka 2014.

gabo

Salim Ahmed aka Gabo

Mwaka jana msanii huyu alitamba na filamu ya ‘Bado Natafuta’ ambayo bado inaendelea kufanya vizuri sokoni. Mwaka huu Gabo pia ameonekana kwenye filamu nyingi ikiwemo ‘Siri Ya Giningi’ iliyofanya vizuri sokoni akishirikiana na Sabby Angel pamoja na Mzee Korongo. Kinachomfanya muigizaji huyu apendwe ni ule uwezo wake wa kubeba uhusika.

Shamsa Ford

Shamsa_Ford_01

Mwaka jana Shamsa alihit na filamu ya Bado Natafuta akiwa na Gabo. Mwaka huu ameweza kutikisa tena kwa mauzo ya filamu yake ya Chausiku inayodaiwa kufikia rekodi ya mauzo iliyowekwa na marehemu Steven Kanumba kupitia filamu yake ya mwisho, Ndoa Yangu.

Jacob Stephen aka JB

Jb

Mwaka huu, mmiliki wa Jerusalem Films na muongozaji wa filamu nyingi zinazozalishwa na kampuni hiyo, JB ametamba na filamu kama ‘Hukumu ya Ndoa’ na ‘Mikono Salama’ambazo aliziongoza pia. Filamu zingine alizoziongoza ni pamoja ‘Wageni Wangu’ pamoja na ‘Chausiku’.

Salma Jabu aka Nisha

nishaaaa

Nisha ambaye amewahi kutamba na filamu kama Tikisa, Pusi na Paku mwaka huu mwanadada huyo aliachia filamu ya komedi, Zena na Betina inayofanya vizuri sokoni.

Jacqueline Wolper

tom_boy 22

Pamoja na hivi karibuni kuiambia Bongo5 kuwa bado yupo benchi kucheza filamu zake binafsi kutokana na mapato kuwa finyu, mwaka huu alitoka na filamu ya Tom Boy. Pia ameokana kwenye filamu ya VIP iliyoingia sokoni October.

Irene Uwoya

irene-uwoya

Mwaka huu Irene ameonekana kwenye filamu kama JAMAL na Nesi Bandia ambazo zote zimefanya vizuri sokoni.

King Majuto

Mzee-Majuto-akifurahia-ushindi

Mzee Majuto anaendelea kufanya vizuri sokoni kutokana na filamu kama Duplicate, Chungu Kimoja, Nahama na zingine.

Vincent Kigosi aka Ray

Ray

Ray kupitia kampuni yake, RJ Company ameendelea kufanya vizuri na hivi karibuni aliachia filamu ya VIP akiwa na Wolper Salha na wengine.

Cloud

ivm5282

Cloud ameendelea kufanya filamu zenye visa vya kuvutia kama Fundi Selemala na Doctor Max zilizotoka mwaka huu.

4_days_mission

Ringo na Tin White

Hii ni timu ya watu wawili. Wasanii hawa wa vichekesho wanapendwa sana na hata kazi zao zinapoingia sokoni huuza vyema. Mwaka huu walitoa filamu kama Utani na 4 Days Mission.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents