Burudani

Wasanii hawa wa UK wajitoa kutumbuiza katika sherehe za kuapishwa Donald Trump

Waimbaji wa Uingereza, Rebecca Ferguson na Charlotte Church waliotarajiwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump wamejitoa.

Imedaiwa kuwa sababu ya Rebecca kujitoa kutumbuiza ni baada ya kubainika kutaka kuimba wimbo wa ‘Strange Fruit’ ulioimbwa na Billie Holiday katika sherehe hizo ambao umeandikwa katika miaka ya 1930 kuhusiana na ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Baada ya kusambaa taarifa za kujitoa kutumbuiza katika sherehe hizo, Rebecca kupitia tovuti yake ameandika:

I wasn’t comfortable with the song choice made on my behalf, and although I’m very blessed to have a gift that gives me amazing opportunities, as a mother and an artist, I had to defend my stance. That is why I made the decision to sing Strange Fruit when I was invited. I requested to sing Strange Fruit, as I felt it was the only song that would not compromise my artistic integrity and also as somebody who has a lot of love for all people, but has a special empathy as well for African American people and the #blacklivesmatter movement, I wanted to create a moment of pause for people to reflect.

Naye Charlotte kupitia mtandao wake wa Twitter aliandika, “@realDonaldTrump Your staff have asked me to sing at your inauguration, a simple Internet search would show I think you’re a tyrant. Bye????????????????.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents