Burudani

Waraka wa Jcb kwa Waislam kote duniani

jcb_wife2

Mimi jacob makalla aka Jcb msanii wa hip hop kutoka Arusha nachukuwa wakati huu kuwaomba radhi ndugu zangu waislam kote duniani, kwa mimi hapa kutumia maneno ya Quran, kwenye nyimbo yangu niliyo irekodi miaka kama mitatu iliyo pita.

Sikuwa na nia mbaya wakati nafanya hivyo,sikuwa na ufahamu wa hayo mambo wakati nafanya hivyo nilidhani namshukuru mungu,kumbeni haramu katika dini ya kislam kuweka maneno ya Qur ana kwenye nyimbo.

Naombeni msamaha ndugu zangu waislam sitarudia tena kufanya hivyo na nitawahimiza, wasanii wenzangu kutofanya hivyo kabisa kwani ni vibaya sana kwa dini ya kislam ni haramu kabisa.

Kwa kweli nimejifunza mengi sana katika hiki kipindi ambacho kwangu ni kigumu sana,hiyo nyimbo sikuwahi kuipeleka redioni kabisa bali imevuja bila mimi kujua.

Nawaombeni ndugu zangu watanzania walikuwa na nyimbo yangu inayo anza na maneno ya kuruhani waifute kama ni kwenye simu au compture popote pale kwani ni haramu,hiyo nyimbo niliimba na ibra da hasla pamoja na salum aka kingston,wote kwa ujumla tunawata radhi tena wazazi wetu kaka na dada zetu pamoja na wadogo zetu wote tulio wa kerai kwa sisi kufanya hivyo,hatukuwa na nia mbaya…ni shetani tu alitupitia

jcb

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents