Habari

Wapi nyimbo za Christmas za Bongo Flava/Kiswahili?

Mwezi December kila mwaka ni mwezi maarufu wa likizo, sikukuu na bata. Baadhi ya wanamuziki duniani kote wamewahi kukitumia kipindi hiki kurekodi nyimbo za Christmas na mwaka mpya.

Ndio maana nyimbo za wasanii kama Jim Reeves, Elvis Presley, Mariah Carey, Boney M, Jessica Simpsons, Justin Bieber, na wengine hupigwa sana katika kipindi kama hiki na ambazo hutengeneza hisia nzuri na ya furaha kwa watu wengi.

Lakini swali kubwa ni kwanini wasanii wa Bongo Flava na wanaofanya muziki wa aina nyingine nchini hushindwa kukitumia kipindi hiki kutunga nyimbo ama albam za Christmas ambazo kwa hakika zikiwepo basi hudumu milele kwakuwa Christmas ipo kila mwaka. Kipi kigumu kwa waimbaji wa Tanzania kuingia studio kutunga na kurekodi nyimbo nzuri kwa ajili ya msimu huu wa dhahabu?

Sababu kubwa hapa ni wengi kushindwa kufahamu umuhimu wa nyimbo za Christmas za Kiswahili ambazo zingeweza kuwaburudisha hata wananchi wengi wasiojua Kiingereza kwakuwa nyimbo nyingi zilizoeleka zipo katika lugha hiyo. Hatuwezi kusema kamwe kuwa hawana uwezo wa kutunga nyimbo hizo. Kwanini panapotokea msiba wa msanii mwenzao huwa rahisi kuingia studio na kurekodi nyimbo nzuri kumuenzi?

Utajiskiaje kusikia wimbo wa Ben Pol, Ali Kiba, Diamond, Ommy Dimpoz, Lady Jaydee na wengine ukizungumzia Christmas?

Ni raha hata kama utaimbwa na msanii wa dini ya kiislam kwakuwa pamoja na kuwa ni sikukuu ya wakristu, Christmas imegeuka kuwa ni sikukuu kubwa ya watu wa kila dini.

Ni muda sasa wa kuwa na nyimbo za Christmas za Kiswahili tena zilizoimbwa na wasanii wanaotamba sasa, wasanii changamkeni na kutengeneza historia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents