Bongo Movie

Wankota kuja na tamthilia yake mpya ‘Uaridi’, itarushwa TBC 1

Wankota Kapunda mwandishi wa miswada ya filamu (Film script) amekamilisha muswada wake wa kwanza kwa ajili ya tamthilia ambayo ameipa jina la Uaridi.

Wankota akiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo

Akiongea na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo akiwa nyumbani kwake Mbezi, Wankota alisema kuwa maandalizi ya tamthilia hiyo yamekamilika na punde crew inatarajia kuanza kufanya urekodiji wa kazi hiyo na utafanyika hapa hapa jijini Dar es Salaam.

“Awali nilifanikiwa kuandika filamu lakini kutokana na gharama zake kuwa kubwa na kuangalia hali ya soko nikarudi nyuma kidogo nikaandika script ya Series ya Uaridi na imefanikiwa sana na maandalizi yanakwenda vinzuri,”alisema Wankota.

Tamthilia hiyo inatarajiwa kuruka katika televisheni ya Taifa TBC 1, na hatua za awali zimekamilika na anatamba kuwa ni tamthilia ya kipekee.

Wankota ni mwandishi mwenye kipaji cha kipekee kabisa kwani pamoja na tatizo la kupooza sehemu kubwa ya mwili lakini ana uwezo wa kuandika script kwa kutumia ulimi tu, mwanadada alipata ajali ya kugongwa na gari siku ya mahafali ya kumaliza kidato cha sita katika shule ya Sekondari Korongwe.

Source: filamucentral

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents