Habari

Wanawake ndio wenye maambukizi zaidi ya VVU nchini

Tanzania imeadhimisha siku ya Ukimwi duniani kwa kuzindua bodi na mfuko maalum wa ukusanyaji wa rasilimali za mapambano dhidi ya UKIMWI ambapo inakadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni moja na laki tano wanaishi na virusi vya Ukimwi nchini.

world-aids-day

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama katika siku ya maadhimisho hayo hulenga kuwakumbuka wahanga wa janga la Ukimwi pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa huo amesema maambukizi ya ukimwi Tanzania bara ni asilimia 5.3 ambapo wanawake wameonekana wakiongoza katika kupata maambukizi hayo ukilinganisha na wanaume.

Aidha Muhagama alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.

“Sasa kuathirika kwa wanawake na janga hili ni asilimia 6.2 ambapo wanaume ni asilimia 3.8 lakini vilevile inakadiriwa kuwa kuna watu takribani 1,538,882 wanaoishi na VVU katika nchi yetu ya Tanzania,” alisema Muhagama.

Hata hivyo Waziri Muhagama aliweza kutoa ufafanuzi juu ya mfuko unaozinduliwa alisema umepitishwa na sheria ya Bunge namba 6 ya mwaka 2015 lengo likiwa ni kukusanya mapato ya ndani ya wenye virusi vya Ukimwi.

“Kila Mtanzania ana wajibu wa kuokoa maisha yake na maisha ya mwenzake kuhakikisha anakuwa ni sehemu ya kukusanya rasimali za mfuko huu ili kupambana na tatizo la ukimwi katika nchi yetu ya Tanzania,” alisema.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents