Burudani

Wanaume wanadhani ukioa mtu wa kanisani umeoa malaika ambaye hakosei – Bahati Bukuku

Msanii wa muziki wa Injili, Bahati Bukuku amefunguka na kuweka wazi kuwa ndoa ilimshinda na kusema katika harakati za maisha yeye alipishana na aliyekuwa mume wake kufikia hatua ya kutengana na sasa kila mmoja kuishi kivyake.

Muimbaji huyo alisema wimbo wake wa ‘Dunia haina huruma’ si kama alimwimbia huyo aliyekuwa mume wake bali anakiri kuwa ni kisa cha kweli kilichotokea lakini hayo mambo aliyekuwa mumewe alikuwa hayafanyi.

“Aliyewahi kuwa mume wangu hakufanya hilo tukio ila kile kisa ni kweli kilitokea sehemu, lakini aliyekuwa mume wangu hakuwa na matatizo haya, ila tu katika harakati zetu za maisha kuna kupishana hivyo nilipishana naye tu. Siwezi kuongea uongo kwa mtu aliyekuwa mume wangu, hata nikiandika kitabu siwezi kuruka hili popote nikisimama nitasema niliolewa ndoa ikanishinda” Bahati alikiambia Kikaango cha EATV.

Kuhusu skendo kuwa ndoa nyingi za “watu wa dini” hazidumu, Bahati amesema wanaume wengi wanakosea kufikiri kuwa wakioa wanawake ambao ni watu wa dini au watu wa injili kama yeye, wanakuwa wameoa watu wasio na makosa.

“Wengi hudhani ukioa mtu wa kanisani umeoa malaika ambaye hakosei, sasa wakishaanza maisha anakuta tofauti, hapo ndipo ndoa inaweza kuvunjika, jama hata sisi ni binadamu pia” Alisema Bahati
Baadhi ya mashabiki walitaka kujua endapo alipata watoto katika ndoa hiyo, ambapo Bahati alikataa kuongea chochote kuhusu yeye kuwa na watot au la, na kusema kuwa hayuko tayari kuongea chochote huku akisema kuwa ana watoto wengi
“Hili swala la watoto sitaki kuzungumzia, mimi nina watoto wengi tu, kwahiyo kwenye ndoa yangu nisingependa kuongelea swala la watoto” alisema Bahati.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents