Habari

Wanasayansi wanaamini maziwa ya mende yatakuwa dili siku za usoni, utayanywa?

Timu ya kimataifa ya wanasayansi imegundua virutubisho muhimu vya protini kwenye maziwa ya mende – ndiyo mdudu mende usiyempenda kabisa!

cockroachmilkpic2_1024

Maziwa hayo yana virutubisho mara nne zaidi ya maziwa ya ng’ombe na wanasayansi wamedai kuwa yanaweza kuwa muhimu katika kuwalisha watu wanaongezeka duniani siku za usoni.

Ingawa mende wengi hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera punctate, wameonekana kutoa utomvu unaonekana kama maziwa yenye protini yanayotumika kuwalisha watoto wao.

Ukweli kwamba kumbe wadudu nao hutoa maziwa unastaajabisha lakini kilichowashangaza zaidi watafiti ni kuwa maziwa yao yana nguvu mara tatu zaidi ya ile inayopatikana kwenye maziwa ya kifaru.

Utafiti huo ulifanywa na wanasayansi wa Institute of Stem Cell Biology and Regenerative Medicine ya India.

Soma zaidi habari hii hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents