Michezo

Wanariadha wa Tanzania wanaoenda Olimpiki 2016 wapata ufadhili

Timu ya taifa ya Tanzania katika mchezo wa riadha itakayokwenda kuiwakilisha katika michuano ijayo ya Olimpiki imepata udhamini wa vifaa vya michezo pamoja na fedha za kiasi cha shilingi milioni tano.

160725122419_wanariadha_tz_512x288_bbc_nocredit

Udhamini huo umetolewa na shirika la hifadhi za taifa (Tanapa)kupitia kwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo na kukabidhiwa kwa wachezaji hao. Ufadhili huu una lengo kuisadia timu ya taifa na kuwezesha kufanya vizuri katika michuano ya Olimpiki na pia kusaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania.

Baada ya kupata ufadhili huo Rais wa shirikisho la riadha nchini Antony Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kulipia kadi za bima ya afya ya wachezaji hao na familia zao kwa muda wa mwaka mmoja.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji hao, Alfonce Felix amesema ufadhili huo utawaongezea chachu ya ushindi na kuitangaza nchi. Timu hiyo ya riadha yenye wachezaji wanne inaendelea na maandalizi ya mwisho chini ya kocha wake Francis John katika kambi yake ya West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents