Habari

Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore hayupo tena madarakani

Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore hayupo tena madarakani, msemaji wa jeshi amewaambia waandamaji kwenye mjini mkuu Ouagadougou. Awali Compaore alidai kuwa angejiuzulu baada ya miezi 12 baada ya serikali ya mpito kumaliza muda wake.

blaise

Hata hivyo, upinzani uliendelea kumtaka ajiuzulu kufuatia ujanja wake wa kutaka kurekebisha katiba ili aongeze muda wa kuongoza. Jana waandamaji wenye hasira nchini Burkina Faso walilichoma moto jengo la bunge kufuatia mipango ya rais huyo kutaka kurefusha kipindi chake cha utawala uliodumu kwa miaka 27.

783651-image-1414686736-100-640x480

Mamia ya watu walivuka ulinzi mkali katika jengo la bunge katika mji mkuu Ouagadougou, ambapo walichoma moto magari kabla ya kukivamia kituo cha runinga cha serikali na kisha ikulu. Mtu mmoja aliuawa katika vurugu hizo zilizozuka muda mfupi kabla ya wabunge kupigia kura sheria ambayo ingemwezesha Compaore — aliyeingia madarakani mwaka 1987 kwa mapinduzi kugombea tena nafasi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents