Burudani

Wanamuziki wa Kenya wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwa show (Top 5)

Wakati Diamond Platnumz akiwa ndiye msanii ambaye anaaminika kuwa analipwa pesa nyingi zaidi kwa sasa Tanzania, hawa ndio wanamuziki wa Kenya wanaotoza pesa nyingi zaidi wanapohitajika kufanya show.

Hii ni Top 5 ya wasanii wa Kenya wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwa mujibu wa Gossip Juice.

1.Redsan
Redsan

Hit maker wa ‘Badder than most’, Redsan ndiye amekamata nafasi ya kwanza katika orodha hii. Ili atumbuize kwenye tamasha, Redsan hutoza kuanzia Ksh850, 000 sawa na Tsh 15,446,000 kwa show moja.

2.Jaguar
jaguar-pic

Mwimbaji wa ‘Kioo’, Jaguar ni miongoni mwa wasanii wanaofanya show nyingi za nje kwa sasa, na kwa mujibu wa orodha hii, hutoza kuaniza Ksh 300,000 kwa show sawa na Tshs 5,451,530.

3.Wyre
wyre

Pamoja na collabo nyingi alizofanya na mastaa wa Jamaica akiwemo Alaine, member wa Necessary Noise Wyre aka ‘The Love Child’ hutoza sawa na Jaguar kuanzia Ksh 300,000 tu kwa show.

4.Nonini
nonini

Nafasi ya nne imekamatwa na Godfather wa Genge ambaye ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa Kenya, yeye hutoza kuanzia Ksh 200,000 sawa na Tsh 3,634,360.

5. Sauti Sol
sauti-sol1

Wanaofunga orodha ya top 5 ni boy band yenye members wanne, Sauti Sol ambao kuwapata kwenye show kutamgharimu promota kiasi cha Ksh 500,000 ambayo huigawana sawa, kwa maana hiyo kila mmoja hupata Ksh 125,000. Kwa Tshs ni kama 9,085,800 ambayo kila mmoja hupata 2,271,000 hivi.

Orodha hii inatupa picha ya jinsi muziki wa Afrika Mashariki bado unasafari ndefu kuja kuwanufaisha wasanii tukilinganisha na wasanii wa Nigeria.

Mwishoni mwa mwaka jana (2013) ENCOMIUM Weekly ilitoa orodha ya mastaa wa Naija wanaolipwa pesa nyingi zaidi (Bonyeza hapa), P-Square ndio waliokuwa wakiongoza kwa kutoza Naira milioni 10 sawa na Tshs 98,827,500 kwa show huku wa chini kabisa alitoza kuanzia Naira milioni 1.5 sawa na Tsh14,824,100.

Source: Ghetto Radio

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents