Habari

Wanafunzi wa IFM waishio Kigamboni waandamana kupinga wizi katika maeneo wanayoishi

wanafunzi

Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM waishi maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo wameendamana hadi kwenye ofisi za wizara ulinzi wakidai kuchoshwa na matukio ya wizi katika maeneo wanayoishi.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanachuo hao maandamano hayo yamekuja baada ya kukithiri kwa vitendo vya wizi na udhalilishajini wanaofanyiwa ikiwa ni pamoja na kubakwa ama kuingiliwa kinyume na maumbile na majambazi.

Amedai kuwa vitendo hivyo vimeendelea kutokea mara kwa mara licha ya kuwepo polisi na kambi mbili za jeshi.

“Tena wakikuvamia wanakwambia lete kompyuta mpakato, blackberry ukikataa unaonja kipigo, then unaliwa T**o na nanihii’ amesema mwanachuo huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents