Burudani

Walter Chilambo akiri muziki umekuwa mgumu

Msanii wa muziki na mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Walter Chilambo amesema anakutana na wakati mgumu kwenye muziki.

Walter Chilambo

Walter ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa anajisimamia mwenyewe katika kila kitu hali inayomfanya ashindwe kufanya vitu vyake kwa wakati.

“Unajua sasa hivi kuna changamoto kubwa kwahiyo kuna wakati mgumu, mara huyu kafanya hiki mara huyu kaibuka. Pia kuna watu wanapeana stress lakini mtu inabidi u-stick kwenye upande wako,” amesema msanii huyo. “Ndio maana unakuta mimi na stick kwenye upande wangu na watu wangu pia, najaribu kufanya kile kitu ambacho mimi nakiweza. Siwezi kujikuna sehemu ambayo mkono haufiki, kwahiyo japo tunaenda tunarudi mimi naoga game iko poa tu. Mimi sasa hivi niko mwenyewe sina management, sina usimamizi wowote, kwahiyo inakuwa ni ngumu sana huwezi fanya kila kitu peke yako inakuwa inanipa wakati mgumu sana. Kuna vitu vingine nahitaji msaada kwa sababu peke yangu nakuwa siwezi. Kwahiyo hiyo ni kitu ambayo inanisumbua, unakuta sometime vitu haviendi on time,” aliongeza.

Kwa upande mwingine Walter amezungumzia ujio wa video zake mbili mpya baada ya ukimya katika muziki wake ambao anadai ukimya huyo ulitokana na matamasha mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.

“Yaani nitatoa video mbili, kuna moja ya wimbo wangu uliotoka, kuna mwingine mpya kabisa. Hizi video hazitatoka kwa wakati mmoja zitatoka kwa wakati tofauti tofauti lakini hazitapishana, unajua nataka nifanye mashambulizi baada ya ukimya fulani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents