Habari

Waliochaguliwa kuingia katika usaili wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2014 watajwa

Vijana 40 watakaoshiriki kwenye usaili wa shindano la Maisha Plus na wanawake 30 kwaajili ya usaili wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 wametajwa kushiriki kwenye mchujo wa mwisho kuingia katika kijiji cha Maisha Plus 2014.

Kushoto ni mratibu wa Maisha Plus, Masudi Kipanya wakiwa na Meneja wa mawasiliano na mahusiano Oxfam Sharon Mariwa
Kushoto ni mratibu wa Maisha Plus, Masoud Kipanya akiwa na Meneja wa mawasiliano na mahusiano Oxfam Sharon Mariwa


Jopo la majaji linalohusisha wataalamu wa masuala ya kilimo, ufugaji, usalama wa chakula, sera na utetezi, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vijana na maendeleo ya kijamii pamoja na wanafunzi 17 kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, walipitia form za waombaji wote na kufanikiwa kuwachagua vijana 40 wa Maisha Plus na na majina 30 ya Mama Shujaa wa Chakula.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Azura Kawe Beach jijini Dar es Salaam jana Jumapili, mratibu wa Maisha Plus, Masoud Kipanya alisema baada ya kupatikana vijana 40 kwa upande wa vijana wa MAISHA PLUS, zoezi litaendelea ili kupatikana vijana 20 watakaoingia katika Kijiji chenyewe cha Maisha Plus.

“Vijana wa Maisha Plus watagawanywa katika makundi mawili ya watu 20 na kupelekwa katika vijiji vilivyochaguliwa Iringa na Zanzibar. Huko wataishi pamoja na familia zilizochaguliwa na kutakiwa kuishi maisha sawa na familia hizo.Zoezi kuu litakuwa ni kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa vijiji hivyo kama changamoto za maji,” alisema.

“Baada ya siku 7 wanakijiji watatakiwa kuwapigia kura vijana hao ili kupata jumla ya vijana 9 Zanzibar na 9 Iringa,jumla 18 watakaopelekwa katika kijiji cha Maisha Plus kuungana na wenzao 12 kutoka nchi za Kenya,Burundi,Rwanda na Uganda.”

“Mama Shujaa watapigiwa kura mtandaoni ili kupata washiriki 20 ambao wataingia kijijini Maisha Plus. Zoezi la kupigwa kura litafanyika baada ya uhakiki ‘verification’ pamoja na upigaji picha kuthibitisha taarifa walizojaza kwenye fomu,” alisema Meneja wa mawasiliano na mahusiano Oxfam, Sharon Mariwa.

Washiriki watakopita katika usaili huo wanatarajia kuingia rasmi kwenye cha kijiji cha Maisha Plus mwezi March mwaka huu.

Majina yawaliochaguliwa kuingia kwenye usaili wa Mama Shujaa wa Chakula.

1.Amina Kupera Chikaponya-Mtwara
2.Anna James Yuda-Morogoro
3.Anna Mwanilyela Chrisant-Katavi
4.Bahati Muriga-Mwanza
5,Clara Ancilla Ibihya-Pwani
6.Cristina Kurwa Malale-Zanzibar
7.Dina Rusoti-Mara
8.Dionisia Rashidi Karata-Tanga
9.Doricus Msafiri Shumbi-Singida
10.Edina James-Mbeya
11.Elinuru Moses Pallangyo-Arusha
12.Elizabeth Matayo-Geita
13.Elizabeth Simon-Morogoro
14.Ezeleda Chedego-Dodoma
15.Fredina M.Said- Shinyanga
16.Gladness Ebenezery Mmary-Kilimanjaro
17.Grace G.D.Mahunguka-Karera
18.Janeth Niima-Manyara
19.Kuruthumu Ramadhani Mwegele-Tabora
20.Leah Dominick Mnyambugwe-Dodoma
21.Mary Athanaz Ndasi-Rukwa
22.Mary John Mwanga-Singida
23.Mary Kessy-Dar es salaam
24.Neema Robert –Simiyu
25.Nyachum Haji Ame-Zanzibar
26.Pendo Musa-Morogoro
27.Santina Mapile-Njombe
28.Thereza Kitinga-Mwanza
29.Zaituni Shedrack Kalembi-Kigoma
30.Zamda Daniely Mgonganga-Iringa


Majina ya vijana waliochaguliwa kuingia kwenye usaili wa Maisha Plus
.

1.Adolph Anacleth-Mwanza
2.Agatha Kalesu-Rukwa
3.Ally Thabit –Mwanza
4.Anastazia John-Mara
5.Asunta Mwingira-Dar es salaam
6.Ausi Abdul Moyo-Ruvuma
7.Bakari Khalid –Shinyanga
8.Boniphace Meng’anyi Nyankena-Dar es salaam
9.Charles Daniel –Simiyu
10.Douglas Said Msalu-Arusha
11.Ellymathew Kika-Njome
12.Elizabeth Joachim-Tabora
13.Hahamni Kaite Mwadini-Zanzibar
14.Farida Ally –Pwani
15.Fadhili Isanga-Kilimanjaro
16.Frora John-Singida
17.Fredirick Joseph Ndahani-Singida
18.Hyasinta T.Hokororo- Mtwara
19.Jane Julio Klinga-Iringa
20.John Sylvester Malima-Geita
21.Joyce Jacob Mushy-Arusha
22.Marriam Mosess –Shinyanga
23.Mary Nicholaus Kavishe-Manyara
24.Mbonimpaye N.Nkoronko-Rukwa
25.Mohammed Selemani Lipemba-Lindi
26.Moureene K.Daud –Kagera
27.Nelson Daniel –Dar es salaam
28.Ngoma Abdallah –Kigoma
29.Osama Norman –Mbeya
30.Otilia Selemani Simemi-Mbeya
31.Said Salum –Katavi
32.Salumu Saidi Johari-Mtwara
33.Scholastica Deusidedith-Geita
34.Self Mohammed Salum –Tabora
35.Shaaban Masoud Shaban-Zanzibar
36.Shida Kaneth Mganga-Dodoma
37.Shishira G. Mnzava-Morogoro
38.Thomas P.Mgazwa-Dodoma
39.Yassini Hamisi Suddi-Dar es salaam
40.Zaharani Yusuph Hossen-Tanga

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents