Habari

Wakazi wa Mabibo waomba msaada Tanesco

umeme_nguzo_face

Mvua ya leo imeweza kuzua kizazaa baadhi ya sehemu hasa maeneo ya Mabibo kwa kusababisha nguzo moja, kuilalia nguzo nyingine. Nguzo hiyo ni miongoni mwa nguzo ambazo Tanesco wamekuwa wakiziweka sasa na tayari baadhi ya watu wanasema zimeshaanza kupitisha umeme.


Wananchi wa maeneo hayo ya Mabibo maeneo ya Makutano, wamesema wanaomba Tanesco wafanye haraka kwenda kuinua nguzo hiyo, kwakuwa umeme bado unaendelea kutumika, hivyo ni hatari sana kwakuwa nguzo hiyo  haijajishika vizuri eneo hilo jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya wakazi wa hapo, kwakuwa mvua zinaendelea kunyesha.

umeme_nguzo_tanesco

umeme_nguzo_za_umeme

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents