Habari

Wakazi aja na kanuni kumi za hela


Ukimuuliza Fid Q ni rappers gani anaowakubali zaidi Tanzania hawezi kukosa kumtaja Webiro Wasira aka ‘Wakazi’. Kama Fid kamkubali hatuna shaka kuwa uwezo wake si haba.

Jamaa anatokea pande za Ukonga, Dar es Salaam lakini kwa muda mrefu sana anaishi Chicago, Illinois nchini Marekani.

Katika ulimwengu wa Hip Hop wakazi ni mfalme wa kanda mseto (mixtape). Mpaka sasa ameshaachia mixtape tatu, MYU: Mixtape Ya Ukweli, MYU2 The Return of The Bilingual Beast na MYU3 Welcome To Heartbreak.

Jumapili hii amekuja na kanuni kumi za hela alizoziweka kwenye vina, ambazo ni hizi zifuatazo:

10. Honestly it should be Number 1 Wanasema “chezea MSHAHARA usichezee KAZI”. No, “cheza na FAIDA usichezee MTAJI”

9. Muhimu kuzingatia kabisa. Tumia hela kimahesabu sio kisa umezishika. Kumbuka vipaumbele kabla kitaa hujatisha.

8. Tumia pesa uweze ku make Money. Haujasikia “Scared money don’t make no money”.

7. Hii wengi itawakwaza. Kwenye pesa hapendwi mtu haijalishi hata mother. Huwezi mix DAMU na NOTI

6. Usiweke Mapenzi kwenye kitita. Ukimkopesha Mpenzi kulipwa sahau kabisa.

5. Daima usikiuke makubaliano. Maana wachimba chumvi hawachelewi kukutolea mfano.

4. I know you heard this before. Tumia Pesa ikuzoee bro.

3. Pesa ya Starehe haina Mahesabu. Ndio maana hata wasiona Mishahara wanakula ulabu. Starehe gharama kama hujui watu.

2. Lugha ya Taifa sio Kiswahili. Ukiona Mtu hakuelewi hebu toa Laki Mbili.

1. Pesa sio kitu cha kungoja. Inabidi ulipwe instantly, tena mara moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents