Bongo5 Makala

Waimbaji wa kike wa Tanzania waliotisha katika robo tatu ya mwaka 2014!

Nilipenda kuwa na orodha ya wanamuziki 10 wa kike waliofanya vizuri katika kipindi cha miezi 9 na robo iliyopita, lakini nimegundua kuwa ni wanamuziki wachache sana wa kike waliofanya vizuri. Hiyo imenisikitisha kidogo kwakuwa bado muziki wa Tanzania umeendelea kutawaliwa na wanaume. Pamoja na hivyo kwenye orodha hiyo chini wapo wasichana waliofanikiwa na kufanya mambo makubwa mwaka huu kuliko wasanii wengi tu wa kiume waliopo kwenye chart.

1.Vanessa Mdee

10458321_868432543175662_3021229218226959496_n

Nakumbukuka mwaka 2013 nilimjumuisha Vanessa Mdee kwenye orodha ya wasanii wa kuwaangalia mwaka huo. Ndio alikuwa ameachia single yake ya kwanza ‘Closer’ baada ya kutoka kushirikishwa kwenye wimbo wa Ommy Dimpoz ‘Me and You’. Unaweza kushangaa kuwa ni mwaka mmoja na miezi kumi tu lakini Vanessa Mdee amepata mafanikio makubwa kuliko wasanii wengi wakongwe.

10290096_930173803668202_5981675724135582724_n

Wimbo wake ‘Come Over’ umemweka katika nafasi nzuri zaidi na kumwezesha kuwashawishi wale waliokuwa na hofu na kipaji chake cha kuimba, japo anakiri kuwa wapo wanaoendelea kuwa na ‘doubt’ na uwezo wake kimuziki.

“Mpaka leo wapo wenye mashaka na mimi,” anasema Vee Money. “Hainikatishi tamaa bali inanipa changamoto kuendelea kuwaprove wrong na kuendelea kufanya kitu kizuri mpaka wale waliokuwa na mashaka na mimi wakubali waseme ‘yeah she is the one’. So I don’t mind a few doubters.”

Vanessa ni msanii ambaye kujituma kwake kumemfanya asioneshe dalili zozote za kupumzika au kubweteka na mafanikio licha ya kuwa na majukumu mengi mengine kama mtangazaji wa redio na TV.

vanessa

Akiumaliza mwaka 2014 na tuzo ya KTMA, Vanessa amefanikiwa kupanda kwenye majukwaa ya show nyingi kubwa za Tanzania ukianzia Kili Music Tour, Fiesta, show za makampuni na na mashirika na zingine. Come Over pamoja na video yake zimempeleka mbali hadi kuingia kwenye charts za vituo kibao vya redio na TV ndani na nje ya nchi.

Vanessa amepata michongo mingi kutokana na muziki wake mwaka huu ikiwa ni pamoja na endorsement ya Airtel, kuchukuliwa kwenye kipindi cha Coke Studio Africa na pia kuteuliwa hivi karibuni kama balozi wa kampuni ya Crown Paints.
Come Over pia imemwezesha mwaka huu kutajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo za AFRIMA.

Akiwa anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake ‘Hawajui’, Vee atakuwa msanii wa kwanza Tanzania kulipwa na kampuni kutangaza brand yake kwenye video hiyo (Product Placement), kitu ambacho hufanywa sana kwenye muziki wa Marekani na kwingine. Pia Vanessa ndiye msanii wa kike anayeangaliwa zaidi na industry ya muziki nje ya Tanzania kwa sasa.

10500529_868432463175670_3067593918842098115_n

“Unajua wasanii wa kike wote wa hapa nyumbani ninawakubali ila namkubali sana Vanessa. Na hata nikikutana naye huwa namwambia kuwa ‘Vanessa unanipa imani sana kuwa tuna mwanamuziki wa kike ambaye naona kabisa anabadilika kila siku na anajituma sana hata akiwa kwenye stage’. Unaona kabisa ana juhudi zaidi maana Vanessa alikuwa akiimba kizungu sana lakini kila siku zinavyoenda anabadilika na anaelewa nini anafanya sio mtu wa kujitoa fahamu,” alisema Diamond Platnumz.

2. Shaa

Shaa

Shaa amebatizwa jina jingine la ‘Malkia wa Uswazi’. Alikuwa kama anajaribu tu lakini nyimbo zake mbili zenye ladha ya chakacha ‘Sugua Gaga’ na ‘Subira’ zimebadilisha kabisa maisha ya kimuziki ya Shaa yaliyokuwa yameanza kuwa na doa.

Kabla ya hapo nyimbo mbili alizotoa na video zake ‘Promise’ na ‘Lava Lava’ zilimfanya arudi kwenye ubao wa kufanyia mipango ili kubadilisha uelekeo.
Hiyo ni kwasababu nyimbo hizo alikuwa akizitegemea kumpeleka mahali lakini zilimdisappoint. Kama unakumbuka alitoa video ya Lava Lava kwa lengo la kutaka kujidhatiti katika soko la kimataifa lakini mambo hayakwenda kama alivyokuwa akitarajia.

10689803_10152770334968570_3455746866143959303_n

Pengine aligundua kuwa ni ngumu kwenda international kama bado hujaweka mizizi thabiti nyumbani kwako. Ndio maana kwa kutoa Sugua Gaga alitaka kuhakikisha kuwa anapata mashabiki wa Uswazi pia ambao kweli amefanikiwa kuwagusa huku pia hata wale wa kishua nao wakimuelewa vizuri tu.

Sugua Gaga ilifungua milango mingi ya kimataifa wa kwanza ukiwa ni ule wa Coke Studio Africa ambako ameonekana kuwa msanii anayeshangiliwa na kupongezwa zaidi.

Shaa-akifanya-yake

Sugua Gaga pia imemfanya aandike historia mpya kwenye muziki wa Tanzania kwa kuwa video ya msanii wa nchi iliyoangaliwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube. Hadi sasa video hiyo imeangaliwa kwa zaidi ya mara 7,145,600!

Mlango mwingine uliofunguka ni wa kupata shavu la kuwa mmoja wa host wa mashindano ya Sakata Mashariki ambako ameendelea kumwagiwa sifa nyingi kwa kazi nzuri. “Lady Shaa is so on top of her game right now! So proud of you boo! Hongeraaaa,” anasema mtangazaji wa Choice FM, Abby.

Tayari amefanya video ya wimbo mwingine uitwao ‘Njoo’ nchini Kenya na amemshirikisha Redsan ambao hakuna shaka utaendelea kumweka vizuri kwenye ramani ya muziki wa Afrika Mashariki kama sio Afrika nzima. “Kama plan A imefeli jaribu plan B…. #NeverGiveUp,” anasema Shaa.

3. Lady Jaydee

1939671_10152347349570025_911943319890253602_n

Nafasi ya Lady Jaydee kimuziki inaendelea kuwepo kila mwaka unaokuja. Mwaka 2014 aliuanza kwa kuachia wimbo ‘Historia’ kutoka kwenye album yake ya ‘Nothing But The Truth’ na kutoa pia video yake. Katika muda huo huo pia mafanikio aliyoyapata mwaka uliopita, yaliendelea kuja mwaka huu na kumwezesha kumiliki gari la kifahari aina ya Range Rover E-Voque.

‘Nasimama’ ulikuwa ni wimbo mpya kwa mwaka huu na ndio wimbo pekee alioutoa hadi sasa japo hiyo haiashirii kuwa hafanyi vizuri redioni. Mwaka huu alifanikiwa kushiriki kwenye wimbo wa kombe la dunia pamoja na wasanii wengine. Amefanya show nyingi kubwa za ndani na nje ya nchi ikiwemo ile ya Machakos nchini Kenya ambako alitumbuiza mbele ya umati wa watu 40,000.

Pamoja na tuzo za KTMA 2014, Jide pia alifanikiwa kutwaa tuzo ya AFRIMMA pamoja na Diamond. Licha ya miezi ya hivi karibuni kuandikwa sana kutokana na kudaiwa kuvunjika kwa ndoa yake na Gadner G Habash na kuwa na meneja mpya (Wakazi), bado Jaydee ameendelea kupata mashavu ya show kubwa kama ile ya hivi karibuni kwenye tuzo za uandishi wa habari Africa za CNN Multichoice.

10711085_10152354957875025_408492672773086530_n

Ameendelea kupata endorsements pia ikiwa ni pamoja na kuungana na Juliana na Jamila waliotajwa kuwa mabalozi wa vipodozi vya Oriflame.

Pia September mwaka huu aliteuliwa kuwa na hospitali ya Marie Stops kuwa balozi wa kampeni ya ‘Chagua Maisha’ inayohamasisha uzazi wa mpango na kupinga mimba za utotoni. Hata hivyo mashabiki wake wanaweza kuwa na muda mrefu wa kusubiri nyimbo zake mpya kwakuwa alikiri kuwa hiki ni kipindi ambacho hana mood ya kuandika nyimbo.

“Huwa nakaa hata miaka 3 au 5 pengine mwezi mmoja au miwili au 6 , yaani huwa haitabiriki, pale inapotokea tu ndio huwa. Natumaini jibu hili ni muafaka na litawaridhisha walio uliza, Poleni kwa kusubiri, i wish ningeweza,” alisema Jide.

4.Linah

Linah na Recho

Kupitia kampuni mpya ya usimamizi, No Flex Zone, mwaka huu Linah amekuwa msanii wa kwanza wa kike kufanya video ya bei kubwa zaidi. Kwa gharama ya dola 30,000, Linah alifanikiwa kushoot video kali ya wimbo wake ‘Ole Themba’ chini ya muongozaji maarufu, Godfather.

Hicho ni kitu pekee ambacho kimemfanya awe tofauti na wasanii wenzake wa kike mwaka huu. Hata hivyo changamoto inayomkabili ni kama ataweza kuendelea kutoa video zenye ubora wa aina hiyo.

Linah

Pamoja na wimbo huo, Linah ana miradi kadhaa ikiwemo kurudia wimbo wake Diamond ‘Kizaizai’ unaofanya vizuri redioni. Pia mwaka huu alitajwa kuwa balozi wa kampeni ya masuala ya wanawake nchini.

“Nimechaguliwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba kupitia kampuni ya Angels Moment ambayo ipo chini ya Mke wa Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, Bi Naima Malima,” alisema.

“Nitakuwa nikizunguka mikoa mbalimbali maana kuna kampeni ambayo mie ndo nitakuwa nikihamasisha inahusu mwanamke na uchumi ambayo inakuwa inahusu pamoja na wasichana ndio maana pia wakaniteua mimi kuwa balozi.”

5. Mwasiti

mwasiti

Mwaka huu Mwasiti ameachia ngoma moja tu ‘Serebuka’ ambayo alitoa pia na video yake. Serebuka imefanya vizuri redioni na kwenye TV pia. Sauti yake ilisikika zaidi kwenye ‘Nishike Mkono’ aliyoshirikishwa na D-Knob.

Wakati wasanii wengine kama Vanessa na Shaa wakiwa na msingi mzuri nje ya Tanzania, Mwasiti ana mkakati tofauti wa kuunjenga wake.

“Mimi plan yangu katika muziki ili kwenda kimataifa ni kufanya matamasha makubwa sana, sio kukutana kwenye show sijui wapi na wapi hapana! Mara nyingi naangalia show zangu nyingi ziwe za matamasha. Kuna wanamuziki wakubwa wa Tanzania hamuwaoni wakifanya hizo show za kawaida, kumbe nimegundua nje ya mipaka yetu wanafanya mambo makubwa sana. Huu ni mtazamo katika muziki ili uende kimataifa kwa kutumia njia tofauti na ambao wanazitumia wasanii mbalimbali, mimi nitakuwa nikiomba kushiriki katika matamasha makubwa ambayo na hakika yatanifikisha mbali sana,” alisema Mwasiti.

Pamoja na muziki, Mwasiti ameendelea kufanya shughuli za kijamii na alichaguliwa kuwa balozi wa kampeni ya ‘Stand Up For African Mothers’.

6.Shilole

Shilole wakiwa amebambiwa na mpenzi wake Nuh

Mwaka huu Shilole alimake headlines kwa video yake ya Chuna Buzi iliyoongozwa na Nisher. Pia amekuwa msanii aliyefanya show nyingi na kupanda majukwaa makubwa kama Fiesta na Kilimanjaro Music Tour.

Wimbo wake ‘Namchukua’ nao umeendelea kufanya vizuri na video yake iliyofanyika nchini Kenya ilizinduliwa hivi karibuni.

7.Meninah

meninah

Katika kundi la wasichana watatu wa Shosteez, ni Meninah pekee ndiye anayeendelea kujituma na kutoonesha dalili za kukata tamaa.

Alisafiri hadi nchini Kenya kwenda kushoot video ya wimbo wake ‘Kakopi Kapesti’ ambao umekuwa ukifanya vizuri. Ameendelea kujifua zaidi katika uchezaji muziki na kuna kila dalili kuwa akipata ‘right tone’ anaweza kuanza kuyafikia mafanikio ya dada zake.

8. Dayna

dayna video

Kwa wanaomfahamu Dayna Nyange, watakubaliana nami kuwa ni msichana anayejituma sana. Tuseme tu labda hajapata bahati kama waliyopata wasanii wengine au kutokuwa na uongozi unaozijua njia za muziki vizuri, lakini msichana huyu kutoka Morogoro ana kipaji cha kuimba.

Skendo ya kuchukuliwa beat ya wimbo wake uliokuja kutumiwa na Diamond kufanya hit ya ‘Number One’, hakukumpotezea imani yake katika muziki. Wimbo na video yake ya ‘I Do’ umekuwa ukifanya vizuri miezi ya hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents