Habari

Wahu akanusha kumuimbia mumewe kwenye ‘Liar”

Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya Wahu amezikanusha story kuwa amemlenga mumewe kwenye wimbo wake Liar.

Kwa muda mrefu wapenzi wa muziki nchini humo wamekuwa wakihisi kuwa anayeambiwa ‘mwongo’ kwenye ngoma hiyo ni mume wake David Mathenge, aka Nameless, ambaye ni maarufu sana kwa mashabiki wa kike.

Katika interview aliyofanya na kituo cha radio cha Easy FM Wahu amesema kisa hicho ni cha kutunga.

“Kila mtu anaendelea kusema, aya, maze sema tu ukweli, you know. (The liar) ni uhusika wa kutunga lakini unaozungumzia mambo yanayotokea. Si unajua watu ni waongo,” alifafanua.

Wimbo huo kutoka kwa mshindi huyo wa tuzo za MTV, Wahu Kagwi umetengenezwa na producer maarufu nchini Kenya RKAY.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents