Michezo

Wahispania wampigia saluti Faridi Musa

Baada ya kufuzu majaribio nchini Hispania, Faridi Musa arejea nchini na matumaini makubwa.

IMG_9443

Mwanzoni mwa mwezi Aprili, mchezaji huyo wa Azam FC alifanikiwa kuelekea nchini Hispania kufanya majaribio kwenye timu ya Club Deportivo Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo maarufu kama Segunda Division.

Akiongea na mtandao wa timu hiyo baada ya kuwasili nchini jana akitokea Hispania, Faridi alisema Farid alisema amekutana na changamoto nyingi sana alipokuwa kwenye majaribio ndani ya kikosi hicho hadi kufuzu lakini tayari ameshazoea.

“Najisikia vizuri sana kufuzu majaribio na namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa hatua niliyofika, watu wa kule Hispania wameonyesha kunikubali sana na najivunia kwa hilo kiukweli nimefurahishwa na hilo sana, kwa hiyo mimi ni juhudi tu nitakazoziongeza kwenye mazoezi kwani malengo ninayoyataka mimi na sehemu ninayotaka nifike bado sana na ndio maana napambana sana niwezavyo,” alisema.

Kwa sasa kinachosubiriwa ni kufanyika kwa makubaliano kati ya timu ya Azam Fc na Club Deportivo ili Farid Musa aende kujiunga kucheza soka la Hispania msimu ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents