Habari

Wafungwa 26 wafariki dunia katika vurugu zilizotokea gerezani nchini Brazil

Wafungwa wapatao 26 wameripotiwa kufariki dunia katika vurugu zilizotokea katika gereza la AlcaƧuz lililopo katika eneo la Rio Grande do Norte, Brazil.

Imedaiwa kuwa vurugu hizo zilitokea siku ya Jumamosi mchana na zilidumu kwa muda wa masaa 14 ambapo zilimalizika mapema siku ya Jumapili.

Wakati huo huo imeripotiwa kuwa maiti tatu za wafungwa hao waliofariki zilikuwa zimekatwa vichwa vyao. Hii ni mara ya tatu kwa mgomo mkubwa kama huu kujitokeza kwenye magereza ya nchini Brazil ikiwemo kwenye gereza la Anisio Jobim na Manaus ambapo inadaiwa kuwa vurugu hizo huanzishwa na vikundi vya uzaji wa madawa ya kulevya.

Mpaka sasa wafungwa wapatao 140 wanadaiwa kufariki dunia katika matukio hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents