Michezo

Wafaransa watatu wasaini mikataba mipya Arsenal

Wachezaji wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francois Coquelin hatimaye wamekubali kuongeza mikataba yao mipya na klabu hiyo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza.


Wachezaji wa Arsenal wakati wa kusaini mikataba mipya

Wachezaji hao wa Kifaransa, beki Koscielny na Giroud wamesaini mikataba hadi 2020, huku mchezaji Coquelin yeye amesaini hadi 2021.

Wafaransa hao wote watatu wamekuwa wachezaji muhimu kwa Arsenal kwa sasa, ambapo Giroud amekuwa gumzo kwa kufunga mabao manne katika michezo minne iliyopita, kujumuisha na bao la kiufundi ‘Scorpion Goal’ alilofunga hivi karibuni kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents