Habari

Wafanyakazi 25 wa Quality Group kujieleza leo katika ofisi za uhamiaji

Hivi karibuni mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, alituhumiwa na ofisi ya uhamiaji kuajiri wafanyakazi 25 wa kampuni yake ya Quality Group wanaowafanya kazi bila vibali. Leo wafanyakazi hao wataanza kujieleza kwa maandishi katika ofisi za uhamiaji.

Ofisa uhamiaji Mkoa, John Msumule amesema uhamiaji haijawakamata wafanyakazi hao, isipokuwa inashikilia hati zao za kusafiria.

Alisema “Kesho yaani (leo) tunatarajia kuanza kuwahoji ili watoe maelezo yao, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kuwapeleka mahakamani Jumatatu ili kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukua nafasi yake.”

Sambamba na kuhojiwa kwa wafanyakazi hao, Manji anasubiriwa na kushtakiwa kwa madai ya kuajiri wageni wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents