Michezo

Wachezaji wa Bournemouth watakiwa kulala wakiwa wamevaa miwani

Wachezaji wa klabu ya Bournemouth wamepewa jozi (Pair) za miwani ya rangi ya machungwa (Orange Glasses ) na timu hiyo ili wawe wanaivaa kabla ya kwenda kitandani kwa ajili ya kuboresha usingizi wao.

Klabu hiyo imewaletea wachezaji wake miwani hiyo (SleepSpec) ambayo husaidia kupunguza mwanga wa bluu (Blue Light) unaotoka katika simu , Tablets, TVs.

Mkuu wa idara ya Afya wa Bournemouth,Craig Roberts amesema kuwa miwani hiyo italeta mabadiliko na manufaa yataanza kuonekana hivi karibuni uwanjani.

“Wachezaji wetu wengi wanatumia muda mwingi hotelini kuangalia Tv au kucheza Games katika Computer,” Roberts aliiambia The Sun. “Matokeo ya hii ni kwamba wanapambana kupata usingizi pale wanapoenda kitandani , kitu ambacho kinaleta madhara katika utendaji wao uwanjani.

“Unapolala ndipo mwili unapojirekebisha/Jitengeneza wenyewe. Kama MCHEZAJI hapati usingizi wakutosha , hataweza kucheza katika kiwango cha juu. Tunaamini kwamba kuwapatia wachezaji kutumia ‘SleepSpec’ itawasaidia kupata usingizi vizuri bila ya madhara yoyote. “

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents