Awards

Waandaji wa Kili Music Awards wakutana na vyombo vya habari

Tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards, leo imekutana na wana habari kuendeleza utoaji taarifa zinazohusisha mchakato wa kuwapata washindi katika kila category na kusisitiza kuwa wapenzi wa wanamuziki na kazi zao wafanye hima kwani muda wa kupiga kura unaelekea ukingoni.

IMG_1306

Tarehe 31-Mei-2013 ndio siku ya mwisho ya upigaji kura. Mashabiki mnahimizwa kutumia muda huu wa lala salama kupiga kura kama haukua umepiga kura yako tayari. “Usije ukajilamu kwavile haukupiga kura, una siku chache zilizobaki piga kura kwa kutumia SMS, Email au mtandao wa www.kilitimetz.com.” Vile vile alisisitiza kuwa makini katika upigaji kura ili kutopoteza kura yao. “Hakikisha unatumia kodi sahihi ya msanii au kazi yake kwenye kura yako. Na kwa wale wa email msisahau kuhakiki kura yako, ukishatuma email system inatuma email yenye ‘link’ ya kubofya kuhakiki kura yako”.

Meneja huyo wa bia ya Kilimanjaro na wadhamini wakuu wa Tuzo za Muziki Tanzania, aliongeza kuwa kwa kipindi chote tangu watangazwe wateule kwenye vinyang’anyiro mbali mbali kumekuwa na mapokeo tofauti. “Naomba niahidi tena kwamba kila ushauri ama kukosolewa kwa tuzo hizi sie kwetu ni changamoto na tunapokea. Tunazoweza kurekebisha ama kujumuisha kwenye mchakato tunafanya hivyo. Yote ni kuhakikisha Tuzo hizi zinaendelea kukua katika ngazi ya kimataifa”.

Kavishe pia alimtambulisha kwa mara ya kwanza msemaji wa Academy kwa mwaka huu Nd. Henry Mdimu na kuahidi kwamba kila mwaka kutakuwa na msemaji tofauti atakaechaguliwa na wana Academy wenyewe ili aweze kujibu maswali ama kutoa maelezo ya jinsi Academy inavyofanya kazi. “Tunachojaribu kufanya ni kuweka uwazi zaidi kwa vile Academy inahusisha watu wenye uelewa mpana wa maswala ya muziki, mambo mengine yanayosemwa hawayakubali kwa vile wanajua kazi ya Academy ni ngumu na kamwe haiusishi rushwa wala upendeleo wa aina yeyote”.

Msemaji wa Academy alisisitiza kwama wana Academy huwa hawakutani kabla kupanga matokeo. “Tunaonana pale kwa mara ya kwanza na tunaingia moja kwa moja kwenye mchakato bila kupoteza muda. Tunazingatia vigezo vya uendeshaji ii kuleta ufanisi kwa zoezi zima.”

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe ameshukuru kwa kazi nzuri ya upigaji kura inayoendelea hadi sasa na kuwaomba wananchi wamalizie mchakato huu wa upigaji kura vizuri katika siku chache zilizobaki.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents