Burudani

Voice Wonder wa ‘Nimpende Nani’ ajipanga kurejea tena

Msanii aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Nimpende Nani’, Voice Wonder amedai kuwa anajipanga kuvunja ukimya wake wa muda mrefu.

cf158f93-593e-4046-8a9c-53c38f9c0950

Akiongea na Google In4 kupitia kipindi cha Vibe la Kitaa cha ABM Radio ya Dodoma kinachoendeshwa na Dj Rodger, Wonder amedai kuwa hahofii kurudisha tena nafasi yake kimuziki kwakuwa licha ya muziki kubadilika mchezo anaujua vyema.

Amesema kuwa hakuna anayeweza kubisha kuwa muziki wa Tanzania umetawaliwa na wasanii wawili tu, akimaanisha Diamond na Alikiba na kudai kuwa wengi wameshindwa kufikia ukubwa huo.

Pia anadai alichojifunza kwenye muziki wa sasa ni kuwa idea za nyimbo nyingi zinafanana kuanzia mashairi na melody hivyo hakuna kinachomshtua.

“Mimi nimefanya muziki kipindi kuna watu wazito na nikapenya, akina Juma Nature, Inspekta wa moto, Chilla, Bushoke wa mtoto, Banana, K Bazil na bado unafanya kitu watu wanajua huyu ni Voice, huyu ni Banana, huyu ni Bushoke kunakuwa na tofauti, mtu anasikia anajua huyu ni fulani na bado soko halikuwepo gumu kwa upande wangu. Sioni kama kuna wasanii wawili watatu wanasumbua mimi nikashindwa kupenya pale kati,” amesema.

Muimbaji huyo anayetokea Dodoma, amedai kuwa tayari ana ngoma tatu ambazo amesharekodi ambazo amewashirikisha Christian Bella, Q-Chief na Madee.

Amesisitiza kuwa muziki wake sasa hivi una mabadiliko makubwa kwakuwa amekuwa kimuziki na kiumri.

Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents