Technology

Vodafone Smart Kicka: Kuwa smart kwa simu hii ya bei chee!

Kuna wakati unaweza kujikuta ukitamani kuuza kitu cha thamani ili tu uwe na simu nzuri itakayokuwezesha kwendana sambamba na ulimwengu wa sasa.

kicka

Inaumiza pia kuona marafiki zao wakimiliki simu za kisasa na wakionekana kufurahia mambo mengi huku wewe ukiwa na simu inayofanya kupiga, kupokea simu na kutuma ujumbe tu. Tumeshasikia kuna watu waliokuwa tayari hata kuuza kiungo cha mwili wao ili kupata simu ya iPhone. Lakini ukweli ni kwamba simu za aina hiyo kwa Mtanzania wa kipato cha kawaida ni ndoto kuwa nayo. Au lah, basi watoto hawatavaa, hawataenda shule na familia haitopata chakula.

Kutokana na kuwepo kwa utofauti huo wa kimaslahi katika jamii zetu, kuna makampuni ambayo yameamua kujitolea kuwasaidia kuwapa fursa watu wa kawaida kupata simu za bei ya chee kabisa lakini zinazomwezesha kufanya kile kile anachokifanya mwenye simu ya bei aghali kama iPhone ama Galaxy.

Vodaphone Smart Phone Kicka ni simu ya mfano wa hicho ninachokisema. Sio simu inayoishia kupiga na kupokea simu au kutuma ujumbe mfupi wa pekee yake, bali ni smartphone haswaa inayokuunganisha na huduma za kisasa kama Whatsapp, Instagram, Twitter, Facebook, akaunti za email mbalimbali na application zingine zinazopatikana kiurahisi kabisa kwenye Play Store.

Simu hii yenye urefu wa 112 mm, upana wa 62 mm na uzito wa gram 100, ina camera itakayokuwezesha kutunza kumbukumbu ya matukio muhimu katika maisha yako. Ili kuitumia vizuri camera hii inakubidi kupiga picha katika maeneo yenye mwenge wa kutosha kwakuwa haina flash.

Ina redio ya FM ambayo imewezeshwa pia kurekodi vipindi unavyopenda kuvisikiliza baadaye.

Betri yake inaweza kudumu kwa masaa manane baada ya kuchajiwa (muda ambao baadhi ya smartphones za gharama kubwa haziwezi kuufikia).

Smart Kicka inatumia teknolojia za ya internet ya 2.5G,2.75G,2G,3.5G,3.75G hadi 3G na pia inakuwezesha kuitumia kusambaza internet (Tethering) kwa simu nyingine au computer. Pia inapokea connection ya Wi-Fi iwapo utapenda kupumzisha kutumia data ya kwenye simu.

Memory yake ya ndani ina ukubwa wa MB 4000 na unaweza kuweka inayohamishika hadi kufikia MB 64000.

Kama unahitaji simu ya bei rahisi unayoweza kuitumia kama simu rasmi au ya ziada, basi Smart Kicka inakufaa. Bei yake ni 79,000 tu na inapatikana kwenye maduka yote ya Vodacom nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents