Promotion

Vodacom yaibuka mwajiri bora mwaka 2013

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeshinda tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2013 inayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo.

001
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal (wa pili kushoto) akikabidhi kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim kombe la Mwajiri Bora wa Mwaka 2013 mara baada ya kampuni hiyo kutangazwa kuwa mwajiri bora wa mwaka 2013 iliyotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE). Nyuma ya Makamu wa Rais ni Makamu Mwenyekiti wa ATE Zuhura Sinare. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Vodacom Tuzo hizo zimetolewa Wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na ATE mwishoni mwa wiki. Mbali na ubingwa wa jumla, Mbali na kutangazwa mwajiro bora wa mwaka, Vodacom ilishinda pia
vikombe vingine vitano katika Nyanja tofauti zinazohusu ajira, usimamizi wa rasilimali watu na masilahi ya wafanyakazi

Mbali na kuibuka mshindi wa jumla katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandiliwa na ATE jijini Dar es salaam na kuongozwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Biala, Vodacom pia imeshinda katika maeneo mengine matano tofauti yanayohusiana na masuala ya uajiri, ajira na usimazi wa rasilimali watu kazini.

“Hakika ni furaha kubwa kwa wateja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 ni mara ya kwanza kwa kampuni yetu kuweza kutambuliwa kwa kiwango kikubwa kiasi hiki” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Voacom Tanzaniz Rene Meza.

003
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal (mwenye suti na tai katikati) akimkabidhi Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim kombe la Mwajiri Bora wa Mwaka 2013 baada ya kampuni hiyo kjutangazwa mshindi wa jumla Wakati wa hafla ya waajiri iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kushoto mstari wa nyuma ni Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka na Makame Mwenyekiti wa ATE Zuhura Sinare. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Vodacom.Mbali na kuibuka mshindi wa jumla, Vodacom ilishinda pia vikombe vingine vitano katika maeneo tofauti yanayohusiana na ajira

Pamoja na kuibuka na Tuzo ya Mwajiri bora wa Mwaka 2013, kampuni hiyo pia imeshinda Tuzo nyingiine tano ambazo ni pamoja na: Best Large Enterprise, Leadership and Governance, Human Resource and Management, Workforce Focus na Best Performance Management Systems.Tuzo hizo zinatambulika na Shirika la Kazi la Kimataifa la Umoja wa Mataifa – ILO ambalo kwenye hafla hiyo liliwakilishwa na Mkurugenzi wake Mkuu Guy Ryder.

Meza aliongeza kwa kusema kuwa, ni heshima na fahari kubwa kwa kampuni yake kuona inaendelea kutambulika siku hadi siku, huku akitanabaisha kuwa tuzo hizo ni chachu kwa kampuni yake kuendelea kupanua huduma na uwekezaji wake nchini, na kuwaendeleza zaidi wafanyakazi ili waendelee kutoa huduma sahihi kwa wateja wa mtandao huo na Watanzania kwa ujumla.

005

“Tuzo hizi ni kama chachu kwetu kuendeleza, Uwekezaji kwa wafayakazi wetu, wateja wetu, miundombinu katika mtandao wetu, na kwa jamii inayotuzunguka. Tumefanikiwa kufanya mabadiliko makubwa kwa Watanzania kupitia simu, sasa hawaishii tu kupiga na kupokea simu na pia tumewawezesha kutumia simu zao katika huduma mbalimbali za kifedha na kufanya mengine mengi kupitia mtandao wetu,” alisema Meza.

“Wateja na wafanyakazi wetu ndio nguzo yetu, tutaendelea kuwathamini na kuwaendeleza ili kufikia mafanikio makubwa zaidi ya haya tuliyoyapata leo.”

008
Wafanyakazi wa Vodacom kutoka kushoto Neema Kissanga, Esther Mattle, Charles Mushi, Stephen Kisanko, Shamsa Hamud, Dorothy Mwanyika, Esther – Itule Masala na Salum Mwalim wakiwa katika picha ya pamoja na vikombe na vyeti mbalimbali Vodacom ilivyoshinda wakati wa hafla ya usiku wa waajiri iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) mwishoni mwa wiki

Kutajwa kwa Vodacom kuwa ni mwajirio bora w amwaka 2013 kunakuja siku chache baada ya kampuni hiyo hivi karibuni kutangazwa kuwa ni kampuni ya tatu katika miongoni mwa walipaji kodi wakuu hapa nchini, tuzo iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA Wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi iliyoadhimishwa mwezi
uliopita .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents