Promotion

Vodacom Tanzania yatoa ufafanuzi kuhusiana na kesi iliyofunguliwa dhidi ya Vodacom International Limited

Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC imetoa ufafanuzi kuhusiana na suala la kesi iliyofunguliwa na Moto Matiko Mabanga dhidi ya Vodacom Group Limited , Vodacom Tanzania PLC (“VCT”); Vodacom International Limited (“VIL”), na Vodacom Congo s.p.r.l (“VDRC”).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,Ian Ferrao inasema ,Moto Mabanga amehusisha suala hilo na hisa za kampuni ya Vodacom PLc zinazoendelea kuuzwa kwa umma kwa lengo la kutaka kulipwa deni la Namemco Energy PTY Limited inayodai kuidai Vodacom International Limited (“VIL”)

Vodacom Tanzania PLC inapenda kuufahamisha umma kwamba suala hilo halihusiani na uendeshaji wa shughuli za Vodacom hapa nchini na zoezi la kuuza hisa kwa umma lililozinduliwa hivi karibuni. Zoezi hili linaendelea kama kawaida na litafikia mwisho mnamo Aprili 19,2017,na uongozi wa Vodacom nchini utaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kama ilivyokusudiwa.

Madai ya Mabanga yanahusiana na kampuni ya Vodacom International Limited (“VIL”) na sio Vodacom Tanzania PLC (“VCT”).Kesi hiyo ilianzia katika Mahakama kuu ya Johannesburg na kumalizika vizuri kutokana na hukumu ya Mahakama ya Biashara ya Kinshasa/Gombe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC).

Kutokana na kumalizika kesi hiyo kwa njia ya mahakama, Moto Mabanga ,alifikisha malalamiko yake tena kwenye Baraza la kusuluhisha kesi zinatotokana na migogoro ya kibiashara (ICC) ambalo liliridhia uamuzi wa awali wa hukumu ya mahakama na kumwamuru, Mabanga kulipa gharama za kesi hiyo kiasi cha USD 7 milioni.Kampuni ya Namenco Energy PTY Limited inapinga uamuzi wa kulipa gharama hizo katika Mahakama ya Rufaa ya Paris,nchini Ufaransa.

Mkurugenzi huyo alisema kampuni yake ina imani kubwa na mahakama kuu ya Tanzania kwani itaelewa suala la kesi hii inayoendelea inayoihusu Vodacom International Limited na Namenco Energy PTY Limited ambayo Vodacom Tanzania PLC (“VCT”); haihusiki nayo,alisema Ferrao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents