Habari

Vituo 4 vya utangazaji vyapewa onyo kali na TCRA kwa kukiuka maadili

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu kali kwa vituo vinne vya utangazaji kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia leo (Ijumaa) kupitia taarifa ya habari.

Akitoa adhabu hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vituo hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi wasikilizaji wake

Amevitaja vituo hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents