Habari

Vitu vya kufanya na kutofanya wakati wa likizo yako

Je ulishawahi kufanya likizo ambayo unaendelea kufanya kazi? Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanahitajika sana katika kitengo chako kama mhandisi wa mashine au mitambo fulani. Makosa ambayo wengi hufanya ni kutosikika tena mpaka wakati watakaporudi tena ofisini baada ya kuisha likizo zao.

staycation

Hivyo wengi wetu hujitahidi kutokuwa sehemu ya ofisi wakati wanakuwa wapo likizo, lakini kama wewe ni mtaalam wa jambo fulani unahitaji kujua vitu vya kufanya na kutofanya wakati huo;

Usizime simu yako
Kumbuka kwamba unahitajika hata kama uko likizo hivyo hakikisha unapatikana katika mawasiliano yako. Unapokuwa unapatikana au kupokea simu unaonyesha wewe unajali taaluma na kitengo chako na kwamba uko tayari kuonyesha ushirikiano.

Wajulishe wafanyakazi wenzako ni wakati gani wawasiliane na wewe na kwa Muda gani.
Ni vizuri uwe muwazi ni wakati gani utapatikana kwa simu na muda gani hautapatikana ili wajue wakati wa kutafuta msaada kutoka kwako kama unahitajika wanakupata muda fulani.

Kama una taratibu za msingi katika utendaji wako wajulishe unaowaacha ofisini.
Inawezekana kazi unaofanya ina hatua fulani za kufuata ili jambo liweze kufanyika, unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha hizo hatua na taratibu unaziweka wazi kwa wenzako ili utakapokuwa haupo iwe rahisi kwao kuzifuata na kufanya kazi vizuri bila kuharibu.

Fuatilia ili uweze kujua kama kuna shida katika kitengo chako na Namna ambavyo ungeweza kusaidia ikiwezekana
Watu wengi tukiwa likizo hatutaki kujihusisha na mambo ya kazi hivyo hatufuatilii kazi inakwendaje na kama kuna tatizo tusaidie kwa namna gani. Hebu fikiria kama kuna tatizo kwenye kitengo chako wakati haupo na haujataka kuonyesha ushirikiano utakaporudi ofisini hilo tatizo litakuathiri kwa namna moja ama nyingine. Kabla mambo hayajawa mabaya zaidi tafuta ufumbuzi na namna ambavyo unaweza kusaidia ukiwa likizo.

Kufanya hivyo unajiongezea uthamani wako na watu watapenda kufanya kazi pamoja na wewe na unapokuwa na tatizo utakuwa na watu ambao wako tayari kukusaidia kutafuta ufumbuzi. Kila mtu anahitaji msaada kwa namna moja ama nyingine hivyo kila ukifanyacho fanya kwa usahihi na kwaajili ya wanaokuzunguka pia.

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents