Burudani

Vita kati ya madirector sio jambo la kushangilia hata kidogo – Adam Juma

Muongozaji wa video Adam “AJ” Juma wa Visual Lab/Next Level, amesema kuwa vita katika sanaa baina ya waongozaji wa video na watayarishaji wa muziki huleta chuki na kuididimiza sanaa nzima.

AJ

AJ ambaye ni miongoni mwa madirector wa mwanzo wa Tanzania ameandika ujumbe huu kupitia akaunti yake ya Instagram:

“Hizi vita za katika sanaa za kijinga sana, hazileti maendeleo bali chuki tu. Vita kati ya madirector sio jambo lakushangilia hata kidogo, kwani mtu ukiwa wa kwanza wa pili maana yake nini? Mnapoteza urafiki kwa ummaarufu wa siku mbili. Kitu hiki kilifanyika kwa pfunk na mj, then dunga na mapigo then lamar, wako wapi hawa watu ambao ndio mngongo wa mziki. Ukiwaangalia hawa maproducer wote ni wakali ila ujinga ndio umesabisha ubishani usiokua na maendeleo. Tujifunze kupenda na kuangalia style za wenzetu sio kwa lengo lakusema nani ni mkali au nani ni wakwanza, kwa nia hiyo tutakuza sanaa. Sijawahi hata siku moja kufikiria kwamba nimfunike mtu flani au niwe on top, bali nafanya kwa kadri ya uwezo wangu kuwa tafauti mengine nawaachia watazamaji. Sitaki kufananishwa na mtu yoyote yule kwa uzuri wala ubaya, kama hujaelewa nachokifanya nunua camera fanya wewe. Nawaonya nyie mnaogombana mkiwa mmesahau mlipotoka, UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU. Hakuna aliyebora kati yetu wote tunaudhaifu wetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents