Bongo Movie

Vita dhidi ya waingizaji wa filamu ‘feki’ za nje nchini isihusishwe na siasa – JB

Ikiwa ni siku moja toka biashara ya filamu ‘feki’ za nje zipigwe marufuku mpaka pale wafanyabiashara wa filamu hizo watakapokamilisha taratibu za ulipaji wa kodi, mengi yameendelea kuibuka, ikiwa ni pamoja na wasanii ambao walihusika kwenye kampeni hiyo kuambiwa wanatumika kisisasa.

Jacob Stephan ‘JB’ akiwa na mashabiki wake wa filamu Kariakoo jijini Dar es salaam

Wasanii hao wakiongozwa na JB, Jumatano hii waliungana na ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam kufanya opesheni hiyo ndani ya soko la Kariakoo kwa madai filamu hizo zinawanyonya wasanii wa filamu wa ndani kwa kuwa zinauzwa bila kulipiwa kodi wakati wao filamu zao zinalipiwa kodi.

JB amedai amesikitishwa kuona baadhi ya watu wanalihusisha tukio hilo na siasa.

“Ndugu zangu kuna jambo naomba niongee na nyinyi, hivi mnajua tunayoyalilia ni maisha yetu, kwa nini kila kitu mnahusisha na siasa? Hivi ni haki mimi nitozwe 30% ya pato langu mwingine asitozwe?,” aliandika JB Instagram.

“Kwenye shida mimi sitajali nani ananisaidia ilimradi anagusa maslahi yangu, ugali wangu, ninakiri sinema zetu zina mapungufu mengi lakini hiyo siyo sababu za kuacha kudai haki zetu. Ni kama mgonjwa akiumwa leo anapelekwa kwa mganga kesho anapelekwa kuombewa anatetea roho yake. Nawaomba sana hatukatai mkitusema kuwa movie zetu zina matatizo lakini ngoja tumalize hili, tusichanganye, na pia hakuna aliye sema zifungiwe hapana zifate utaratibu kama sisi tunavyo fata. Hizo hizo movie zetu mbovu ndio zinatuwezesha kuishi,” aliongeza.

“Lakini pia lazima mfahamu biashara hii ni kubwa kuliko mnavyodhania, movie 2 zinanitosha kuishi kwa mwaka mzima, ushawaza ni kiasi gani mimi pamoja na kushiriki mapambano haya ni kama nimemaliza muda wangu kwenye kazi hii nimebakiza movie 1 tu. Je udhani mwanao au ndugu yako naye anaweza kuingia huku?. Tukiiponda tasnia huniharibii mimi tu, unaharibu maisha ya watu wengi wajao ambao watafanya vizuri zaidi yetu,” alifafanua zaidi.

Sakata hili limewagawa wasanii wa filamu nchini mara mbili. Wapo ambao wanaamini njia hiyo itasaidia kukuza tasnia ya filamu huku wengine wakipinga njia hiyo kwa madai kua siyo sahihi kwani filamu za nje zilikuwa nchini toka zamani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents