Habari

Viroba vyapigwa marufuku rasmi kuanzia Machi Mosi

By  | 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi Mosi, mwaka huu Serikali itapiga marufuku pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.

Ametoa kauli hiyo wakati akizumgumza na maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara.

“Kuanzia tarehe 1 mwezi 3 ni marufuku kuzaliwa viroba , tutakae mkuta na viroba sisi na yeye, wanaotengeneza pombe watengeneze pombe waziweke katika ukubwa unaokubalika. Sasa hivi viroba vinatumika kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, watoto wa shule za msingi wanatumia kwa sababu ni rahisi kuweka mfukoni na kutembea navyo.

Hivi karibuni bunge lilijadili suala la usitishaji wa pombe aina ya hiyo na kuahidi lipo katika mchakato.

By: Emmy Mwaipopo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments