Michezo

Viongozi wa klabu Simba wawasimamisha Kiemba, Kisiga na Chanongo

Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba imetangaza kuwasimamisha wachezaji wake watatu ambao ni HARUNA CHANONGO, AMRI KIEMBA na SHAABAN KISIGA kwa tuhuma za kuhusika kuihujumu timu na kuisababishia matokeo yasiyoridhisha.

FOS

Kamati hiyo pia inawachunguza kocha msaidizi Suleiman Matola pamoja na Daktari wa timu kwa kuhusika katika hujuma hizo. Kamati hiyo imetoa mechi TATU kwa benchi zima la ufundi kuhakikisha timu inafanya vizuri kwa kupata kati ya pointi 7 hadi 9 vinginevyo italifanyia mabadiliko makubwa benchi hilo.

Katika msimu huu wa 2014/15, Simba imecheza mechi 5, imefunga magoli 5, imefungwa magoli 5, imetoka sare mechi 5 na ina point 5.

Source: Mwanaspoti

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents