Habari

Video: Vigogo wa kisiasa akiwemo Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu sasa kukatwa kodi

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema sio wabunge peke yake ambao watatozwa kodi mafao ya kiinua mgongo chao bali viongozi wote wa kisiasa watatozwa kodi katika mafao hayo akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.
MPANGOBUNGE

Akijibu leo hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Waziri Mpango amesema viongozi wa kisiasa watakao tozwa kodi hiyo yupo pia Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mawaziri na manaibu waziri.

Viongozi wengine ni Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, wabunge, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents