BurudaniVideos

Videos: Biafra kuwaka moto

Wakilisha 31

Zaidi ya wasanii 20 wa kizazi kipya nchini Tanzania juzi walipanda katika jukwaa moja kuhamasisha vijana kuhusu upigaji wa kura ifikapo siku ya uchaguzi mkuu wa taifa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 nchini kote.

Tamasha hilo ambalo lilipewa jina la “Wakilisha 31” ikimaanisha tarehe ya uchaguzi mkuu mwisho wa mwezi huu, liliandaliwa rasmi kuwapa hamasa wananchi, hususan vijana kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili ijayo kupiga kura katika uchaguzi mkuu.

Moja kati ya vivutio katika tamasha hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya Biafra, maeneo ya kinondoni Dar es Salaam, ilikuwa wasanii walemavu walioweza kuteka hisia za mashabiki wa muziki wa bongo fleva baada ya kumudu vyema kuburudisha na nyimbo yake.

Pia msanii mlemavu wa mikono na miguu aliweza kuwapagawisha mashabiki wa muziki kwa jitihada zake za kucheza na kuimba ikiwemo kubinuka sarakasi ambapo zaidi ya wakazi elfu tano wa jijini Dar-Es-Salaam walihudhuria na kushuhudia.

Wakilisha 31

Wasanii wengine walioshiriki tamasha hilo la Wakilisha 31 ni pamoja na Keisha, Jay Mo, Jaffari, Mataluma, Amini, Roma,  Mwana FA, Fid Q, Kala Pina, kikundi cha muziki na densi THT, Chidi Benz na Banana Zoro ambaye alipanda stejini na Baba yake mzazi mzee Zahir Ally Zahor.

{hwdvs-player}id=1230|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1229|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1228|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1227|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1226|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1225|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents