Burudani

Video/Picha: Wema Sepetu na mama yake wabwaga manyanga CCM, wahamia rasmi Chadema

Malkia wa filamu nchini Wema Sepetu na Mama yake hatimaye wamevunja ukimya na kuthibitisha kuwa wamehama CCM na kwenda Chadema.

Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii nyumbani kwao Sinza jijini Dar es Salaam, Wema amesema chanzo cha kuhama chama hicho ni kutokana na kufanyiwa vitendo dhahiri vya kuonewa huku akipinga kutumia hasira kuchukua maamuzi hayo ya kukihama chama hicho kutokana na jina lake kutajwa kwenye orodha ya watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

“Nimeamua kufanya uamuzi wa kuhama chama cha Mapinduzi na hivi sasa nataka kuhamia Chadema. Sitaki ionekane kwamba labda nimepata hasira kulingana na hizi tuhuma za hapa katikati ambazo zimenikabili. Lakini nataka nionekane nimefanya maamuzi kama binadamu yeyote ambaye angeweza kufanya. Nadhani wote mnajua kuwa nilishawahi kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi, nilikuwa nalisema kwa kujiproud nikiwa nina uaminifu mkubwa kwamba mimi nitasimama kama kweli kada wa Chama cha Mapinduzi,” amesema Wema.

“Ndugu zangu nimetuhumiwa hivi karibuni na nilivyokuwa najitoa kama kada nilijitoa maisha yangu, nilijitoa utu wangu, nilipoteza muda wangu kupigania kile ambacho nahisi kwamba kwangu ni sahihi na kwamba one day kitaweza kisinitupe na kikanidhamini kwa kile ambacho nimekifanya. Lakini instead vile nilivyokuwa navitegemea havikutokea, sisemi nilikuwa nafanya ili nije kubebwa kama Princess kama Queen kwa sababu Wema ulijitoa ukikosea usiadhibiwe,” ameongeza.

“Lakini kile kilichotokea kwangu nilikichukulia kama uonevu, nimekaa kimya muda mrefu sio kama nilikuwa nafurahia kilichokuwa kinanitokea, hapana. Nilikuwa bado natafakari na kutafuta where did I wrong ni kitu gani ambacho nimekosa mpaka nimefikia hatua ya kufanyiwa hivi ambavyo nafanyiwa.”

Wema amesisitiza kuwa sababu nyingine iliyomshawishi kuhamia Chadema kwa sababu chama hicho kinapigania demokrasia na uhuru wa watu kutokana na utafiti wake alioufanya na hicho ndicho anachokitaka.

Kwa upande wake mama Wema amesema, “Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi, nimehangaika na mwanagu alivyowekwa ndani na Mhe. Makonda. Kashutumiwa anavuta madawa ya kulenya na anauza madawa ya kulevya, hakuzungumza yeye lakini sasa hivi mimi nguli ndio nazungumza. Muuza madawa ya kulevya anakaa hivi? Kwanza zile siku saba alizowekwa nafikiri sasa hivi tungemtoa kule yuko hoi mahututi anataka apewe tu arosto.”

“Ndani ya Chama cha Mapinduzi sikumuona mtu hata mmoja kuja kusema kwamba kuulizia na hata kunipa pole, kuna viongozi watatu tu ndio walionipigia simu na kuniuliza “Mama Sepetu tatizo ni nini?” nikawaambia mimi hapa sijui tatizo ni nini. Lakini mwanangu amedhalilishwa, ameteswa na mpaka usiku walikuwa wanafuatwa na Makonda mule ndani wapo central.”

“Huyu ambaye alikuwa anamfanyia kazi Makonda zinatoka kwenye mitandao. Kamfanyia kazi Makonda, fanya hivi rusha ili nionekane mimi nimefanya kazi hizi lakini kumbe alikuwa anamtuma mvuta unga. Bado alichoongea cha ukweli bado anawekwa haki za binadamu hazikuzingatiwa. Mtu hata kama una makosa wapo wanaoua wanawekewa dhamana lakini dhamana kwake ilikuwa ni shida.”

“Sasa huu ni wakati wa kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi. Mimi nikiwa kama mama nina uchungu nimeamua nimesema siwezi kuteswa nikiwa ndani ya CCM, mwanangu hawezi kudhalilishwa akiwa ndani ya CCM. Sasa nachotaka kusema jamani CCM mimi sasa basi kulingana na hali halisi ilivyotokea. Tumedhalilishwa vya kutosha, tumenyanyaswa vya kutosha sasa hivi basi.”

Wakati huo huo Mama Wema ameongeza kuwa nyuma yake ana watu 5,000 ambao watamfuata Chadema pamoja na familia yao ya mkoani Singida yenye watu zaidi ya 72 wote wamemuahidi kuwa watajiunga na chama hicho na wote watarudisha kadi za CCM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents