Promotion

Video/Picha: Tusker Lager yazindua kampeni ya ‘Fanya Kweli’

Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries, kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager, Jumatano hii imezindua rasmi kampeni yake mpya ijulikanayo kwa jina la Fanya Kweli.

IMG_6072
Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Steven Gannon (Kulia) na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wakiteta jambo

Fanya Kweli ni kampeni iliyolenga kuwahamasisha watanzania kushiriki katika kutengeneza mafanikio yao. Kampeni hiyo itasherehekea kwa pamoja na watanzania katika kusaidiana ili kufikia kesho iliyo bora kwa kila mmoja.
IMG_6030
Mrembo akiwa amebeba chupa ya Tusker Lager yenye muonekano mpya

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Danken uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Steven Gannon alisema kampeni hiyo haimaanishi kuhamasisha fikra za kimaendeleo peke yake bali pia kuwapongeza wale waliofanikiwa kwa yale waliyoyafanya.

IMG_6075
Kutoka Kulia: Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Steven Gannon, Meneja wa bia ya Tusker, Sialouise Shayo, Meneja Masoko wa Tusker Anitha Msangi Rwehumbiza na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru

“Kwenye kampeni hii ya Fanya Kweli tunakamata ile morali ya Watanzania wa kisasa, tunakamata nguvu ya wajasiriamali wa Tanzania,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru amesema ‘Fanya Kweli’ ni kampeni iliyowezeshwa kwa kiwango cha juu. “Tunatarajia kuwa na vipindi mbalimbali vya redio kila wiki ambapo watu kutoka kada mbalimbali kimaisha watashirikiana na watu waliofanikiwa. Sambamba na hilo wateja wa Tusker watapata nafasi ya kujifunza tukio la Fanya Kweli katika baa mbalimbali na kupitia vyombo mbalimbali,” amesema.

IMG_6018
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru akifafanua kuhusu kampeni ya Fanya Kweli

SBL pia kupitia kinywaji hicho hivi karibuni itazindua application ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kwenye soko la bia ambayo itawashirikisha wateja na shughuli zote za kampeni za Tusker Lager zikazoambatana na zawadi.

IMG_6065
Meneja wa bia ya Tusker, Sialouise Shayo akiongea kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo

IMG_6038

IMG_6047

IMG_6079

IMG_6091

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents