Habari

Video/Picha: Msanii ‘Mimi Mars’ kutoka label ya Vanessa Mdee azindua video ya wimbo wake mpya ‘Sugar’

Msanii mpya wa muziki ‘Mimi Mars’ kutoka label ya Mdee Music ya muimbaji Vanessa Mdee amezindua video yake mpya ya wimbo Sugar.

Mimi Mars akizungumza na waandishi

Uzinduzi huo ambao ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa muziki, umefanyika Ijumaa hii katika Club ya Next Door Masaki jijini Dar es salaam.

Akiongea na Bongo5 wakati wa uzinduzi huyo, Mimi Mars amedai wimbo huo utamtambulisha ramsi kwenye game ya muziki.

“Wimbo unaitwa Sugar na kwanini Sugar ni kwa sababu ukijua mapenzi ni kitu kizuri, mapenzi ni matamu, kwa hiyo ni kama Sukari Sugar,” alisema Mars.

Muimbaji huyo alisema anaishukuru label ya Mdee Music kwa kuona kipaji chake na kuamua kumsupport. Angalia picha.


Wageni mbalimbali wakikaribishwa


Jux akifanya mahojiano


Feza akiwa na Mimi Mars


Barnaba na Mimi Mars


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents