Habari

Video/Picha: Mrisho Mpoto apamba matembezi ya kukomesha ujangili nchini yaliyoandaliwa na ubalozi wa China

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amepamba matembezi ya amani ya kuhamasisha jamii kukomesha mauwaji ya tembo nchini yaliyoandaliwa na Ubalozi wa China nchini.

https://www.facebook.com/mrishompototz/videos/1189483521170574/
Mrisho Mpoto akiimba wimbo maalumu kwajili ya kuhamasisha watu kuachana na ujangili

Matembezi hayo yalianzia Ubalozi wa china Masaki mpaka Sea Cliff Hotel huku ageni rasmi akiwa ni Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa.

Jacqueline Mengi pamoja na Ben Pol ambao ni mabalozi wa Wildaid walikuwepo matembezi hayo.

Akiongea katika matembezi hayo ya amani ya kupinga ujangili hapa nchini, Balozi wa China, Lu Youqing alisema nchi ya China ipo kwenye mkakati wa kupiga marufuku biashara hiyo na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu kumalizika kabisa.

Alisema licha ya nchi zingine kufanya biashara hiyo lakini nchi yao ndio inaonekana kufanya zaidi hali ambayo imeifanya serikali yao kujipanga kuIkosemba kabisa.


Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa

Kwa upande wa Rais mstaafu Benjamin William Mkapa ameitaka serikali kutumia kiasi cha pesa ambacho kinapatikana upitia utalii kwajili ya kuwanufaisha watu ambao wanaishi kando kando na hifadhi hali ambayo alidai itapunguza ujangili.


Mrisho Mpoto akiteta jambo na mmoja kati ya wadau wake wa karibu


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akiwa katika matembezi hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents