BurudaniDiamond Platnumz

Video:Diamond asema BET imempa connection nyingi, ‘ukiacha kuuza muziki kollabo ni kitu ambacho kinasaidia’

Msanii wa muziki Nasib Abdul aka Diamond Platinum amesema kuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za BET nchini Marekani kimempa connection nyinyi za kimuziki pamoja na kollabo ambazo zinaweza zikasaidia zaidi.
Diamond

Akizungumza na waandishi jijini Dar es salaam jana baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K Nyerere akitokea Marekani, Diamond alisema amepata connention nyingi ambazo kwa sasa ni mapema kuziweka wazi.

“Kiukweli nyingi sana, ata wakati nipo njiani nilikuwa naongea na manager kidogo , lakini siyo vizuri kuanza kuvisema sasa hivi, naogopa kivisema sasa hivi kwa sababu uongozi unajua, lakini kiukweli ni vitu vizuri sana, ambavyo ata baadae vikitangazwa watu watafurahi, wataona kweli tunafanya vitu, cha kwanza kabisa muhimu ukiacha kuuza muziki, kollabo ni kitu ambacho kinasaidia , unajua kufanya kollabo na watu wa nje kama tulivyofanya kollabo huku Tanzania, na ikafanya vizuri na ikatupenyesha vizuri Afrika, tukifanya na mtu wa kule ( Marekani) tunaingia kule kiurahisi” Alisema Diamond

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents