Burudani

Video ya wimbo wa Amini ‘Mbeleko’ kutoka wiki hii

Video ya wimbo mpya wa Amini, Mbeleko itatoka wiki hii.

10610975_1513576092234592_1640028390_n

Amini ameiambia Bongo5 kuwa mapokezi ya wimbo huo ni mazuri hivyo video yake lazima ikidhi matarajio ya watu walioupenda wimbo huo.

“Muziki kama huu umefanywa na wasanii wengi, akina Mataluma walifanya mchiriku, Dogo Mfaume na wengine wengi, sisi tunakuja kukazia tu,” amesema. “Kwahiyo ni muziki ambao upo na utaendelea kuwepo. Mapokeo yamekuwa makubwa sana, watu wa mikoani wamekuwa wakinipigia simu kuhusu huu wimbo. Ni kwa siku chache lakini imeweza kuenea mitaani. Pia video imetengenezwa kutokana na maudhui ya wimbo na mazingira pia. Kutoka video itakuwa mapema kusema ila karibuni katika wiki hii hapa mwenyezi Mungu akitupa uhai video itakuwa imeshatoka.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents