Burudani

Video ya ‘No Church in the Wild’ ya Kanye West na Jay-Z yatoka ikiwa na ujumbe mzito

Hatimaye video ya wimbo mpya wa Kanye West na Jay-Z, “No Church in the Wild” jana imetoka.

Video hiyo inawaacha mashabiki na ujumbe mzito hata kama nguli hao wawili hawaonekani kwenye video.

Kwa mujibu wa MTV uamuzi huo wa Kanye na Jay-Z kutooenekana kabisa kwenye video hiyo iliyoongozwa na Romain Gavras umekuwa na faida kwakuwa kama wangeonekana, ujumbe waliotaka kuuwakilisha usingefika kwa walengwa kama walivyotarajia.Muda kidogo kabla ya mdundo haujaanza kusikika, wanaonekana vijana (wengi wanafunzi wa kiafrika wanaosoma jamhuri ya Czech) wakiwa wamevalia vinyago wakitembea kwa ‘slow motion’ kuelekea kwenye ukuta wa polisi waliojiandaa kwa kuvaa nguo maalum kupambana na waandamanaji.

Kichapo kinaanza kikisindikizwa na mlipuko mkubwa wa bomu kwenye mtaa wa mjini mkuu wa Czech Prague. Gavras anaonesha nguvu ya mapambano inayotokea kila kona ya dunia iwe maandamano ya Misri, Libya, Tunisia (mwaka jana) Los Angeles 1992 hata London mwaka 2011.

Waandamaji wasio na woga wanaonekana wakirusha mawe na kupigana na polisi wenye silaha kwa kutumia mikono mitupu. Katika scene moja, polisi anaonekana akimkimbiza kwa farasi mwanamapinduzi mmoja anayeanguka na kuambuliwa kichapo cha ‘rungu.’

Vijana wanaonekana wakipigwa na kuburuzwa chini huku kiitikio kilichokaa kisoul cha Frank Ocean kwenye ngoma hiyo kikisika taratabu juu ya mdundo uliopikwa na Yeezy mwenyewe, “Will he make it out alive?”

Mwisho kabisa mwa video hiyo yenye dakika tano, wapigania uhuru wanaonekana kupata ushindi kwa kiasi fulani.

Hata hivyo, japo wameshinda vita, hakuna mwisho unayomaliza yote, ikimaanisha kuwa mapambano bado yanaendelea.

No Church in the Wild- Jay-Z and Kanye West

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents