Burudani

Video: Wyclef Jean apigwa pingu na polisi akihisiwa kibaka

Wyclef Jean alijikuta akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa jijini Los Angeles, Marekani waliomkamata na kumfunga pingu kwa kumfananisha na kibaka waliyekuwa wakimsaka.

Mwanzilishi huyo wa kundi la The Fugees akiwa na abiria wawili wa kike mmoja akiwa meneja wake, walisimamishwa na polisi wa Los Angeles saa saba na nusu usiku huko West Hollywood. Maafisa hao walidai kuifananisha gari yake na ile iliyotumika kwenye tukio la uporaji maeneo ya jirani.

Wyclef, aliyedai kuwa alikuwa amevaa bandana ya Haiti, alisimamishwa kwasababu kibaka anayehisiwa alikuwa amevaa bandana nyekundu.

“Why am I in Handcuffs!!!!!????? This is what I said to the LAPD after they put me in Handcuffs for mistaken identity,” ameandika Wycleif kwenye video aliyoiweka Instagram.

“I was asked by the police to Put my hands up. Then I was told do not move. I was instantly hand cuffed before being asked to identify myself and before being told why. In the process I said my name and told them they have wrong person,” ameongeza kwenye video nyingine.

“They proceeded to ignore me and I was treated like a criminal. I am sure no father wants his sons or daughters to see him in Handcuffs especially if he is innocent. As some one who has law enforcers in my family, I was appalled by the bahavior of the LAPD.”

Polisi wanasema waliamua kumpiga pingu muimbaji huyo baada ya kuushika mkanda wake. Alifungwa pingu kwa dakika sita na kuachiwa baada ya kuonekana hakuhusika na lolote.

Mhusika halisi wa tukio alidaiwa kukamatwa katika muda huo huo kwa mujibu wa TMZ.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents