BurudaniWema Sepetu

Video: Wema Sepetu aizungumzia filamu yake mpya ‘Family’, aigiza kama mgonjwa wa saratani

Unakumbuka kipindi Wema Sepetu amenyoa kipara na kupiga picha na mchumba wake Diamond Platnumz zilizopata comments na likes nyingi Instagram? Alinyoa kipara kuigiza kama mgonjwa wa saratani kwenye filamu yake mpya iitwayo Family aliyoshirikiana na Aunty Ezekiel.

Wema ameiambia Bongo5 kuwa Family ni filamu tofauti na zile za kibongo ulizozizoea kuziona. “Mimi naimani kuwa tasnia ya bongo movie watu walishazoea mfumo mmoja, story za aina moja, story zetu most of the time mimi huwa naziita story za kwenye makochi na za juice,” alisema.

“Kwasababu unaweza ukashangaa mtu amekaa kwenye kochi yaani yeye story imeenda imerudi wako kwenye makochi tu sebuleni, wamehama sana wameenda chumbani, hawathink out of the box. Na story ziko zilezile, mke sijui hawezi kuzaa, kuna sijui uganga. Sisi tumefanya kwanza research, tukaangalia story ambayo iko different, story ambayo hawajafanya watu wengi. Tumehit target nyingine, it’s about cancer, kwenye hiyo story ni mgonjwa wa cancer na ndio maana kuna kipindi mliniona nimenyoa kabisa kipara. Watu wengi walijiuliza kwanini Wema kanyoa lakini the aim was kudeliver kile kitu ambacho nilitaka kudeliver kuwe kuna uhalisia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents