Burudani

Video: Wasanii wengi wanamiminika kutaka kolabo lakini nawachomolea – G Nako

Msanii wa muziki wa hip hop G Nako amedai bado kuna idadi kubwa ya wasanii wanamiminika kutaka afanye nao kolabo lakini anawachomolea.

Mapema mwaka jana rapper huyo wa Kundi la Weusi alitangaza kupunguza idadi ya kufanya kolabo na wasanii wenzake kwa madai brand yake inaharibika kutokana na kusikika kwenye kazi nyingi za wasanii.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, G Nako amedai licha ya kutoa tangazo hilo mwaka jana lakini bado kuna wasanii wanamsumbua.

“Nimezikataa nyingi sana,” alisema G Nako. “Nawaambia sifanyi kolabo kwa sasa hivi kwa sababu ukizungumzia suala la kufanya kolabo nimefanya nyingi sana, kwa hiyo nikikwambia sifanyi kolabo utanielewa kwamba sifanyi kolabo,”

Hata hivyo rapper huyo amesema mashabiki wake watasikia kolabo chache ambazo yeye ataona zinauzito kwa upande wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents