Diamond Platnumz

Video: Wanafunzi wa Kiswahili chuo kikuu cha Florida na project ya wimbo wa Diamond

Hii ni video ya wanafunzi wa awali wa lugha ya Kiswahili walioshiriki kwenye mradi wa mwaka 2014 uitwao African Language Initiative (AFLI) katika chuo kikuu cha, Gainesville, Florida nchini Marekani. Wakijifunza lugha hiyo kwa miezi sita, waliamua kutengeneza filamu hii fupi kama kumbukumbu ya muda mzuri waliokuwa nao kwenye mradi huo ulioongozwa na Wakenya, Filipo Lubua, John Munyui na Brenda Wawire.

Katika video hiyo ya juu, mwalimu (mwanafunzi anayeigiza nafasi hiyo) wao amewapa kazi ya kufanya kuhusu muziki wa Afrika Mashariki. Wanafunzi hao wanakubaliana kwenda kuongea na mkuu wa chuo kumuomba awape fedha ili wamlete Diamond Platnumz kwenye chuo hicho.

Video ya chini ni fupi ambayo inaonesha kipande walichokuwa wakijifunza kucheza wimbo wa Diamond ‘Number 1’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents