Burudani

Video: Walichosema wabunge na maamuzi ya Waziri Nape kuhusu uvamizi wa Makonda Clouds

By  | 

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye, Jumatatu hii, March 20, alikwenda katika makao makuu ya Clouds Media Group kufuatia taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa kipindi cha Da W’keend Chat Show kurusha kile alichokiita kipindi chake.

Waziri Nape ameunda tume ya uchunguzi ya watu watano watakaongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo, Hassan Abbas, na kutoa masaa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Mkuu wa Mkoa Makonda na kutoa ripoti yake Jumanne hii, March 21, 2017.

Baadaye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii iliwasili katika ofisi za Clouds Media Group na kuzungumza na uongozi wake kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwepo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Peter Serukamba.

Tazama Video zaidi hapa chini

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments